Serikali ya Somalia imetangaza kupiga marufuku kuanzia siku ya Alhamisi programu ya kushiriki video na ujumbe maarufu uliosimbwa ili kuzuia propaganda za “kigaidi”. Tovuti ya kamari mtandaoni pia inalengwa.
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia inashutumu mitandao ya TikTok, Telegram na tovuti ya 1XBET kwa kueneza habari potofu na maudhui hatari kwa nchi.
Machapisho yanayoonyesha, kwa mfano, wasichana na wavulana wakidhulumiwa au kutishiwa, au picha za vurugu, lengo: “kueneza uasherati” na “kupotosha umma”.
Kulingana na wizara hiyo, kupigwa marufuku kwa mitandao hii mitatu kutawezesha “kuharakisha vita (…) dhidi ya magaidi ambao wamemwaga damu ya raia wa Somalia”.
Ili kuzuia propaganda zao, mashirika yanayotoa huduma za mtandao watachangia katika kupiga vita mambo kama hayo. Wizara ya Mawasiliano imewapa hadi Alhamisi ijayo kukataza ufikiaji wa majukwaa hayo matatu, chini ya adhabu ya hatua za kisheria.
Uamuzi huu unakuja katika mkesha wa awamu ya pili muhimu ya mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Al Shabab, kundi la wanamgambo wa Kiislamu ambalo limetoa changamoto kwa serikali kuu mjini Mogadishu kwa zaidi ya miaka kumi na tano. Alhamisi iliyopita, rais wa Somalia alisema anataka kuwaondoa wanamgambo wa Kislamu nchini humo ndani ya kipindi cha miezi mitano ijayo.