Marekani na watetezi wa haki za binadamu Alhamisi wamerudia tena wito wao kuutaka utawala wa Taliban nchini Afghanistan kuwaruhusu wanafunzi wa kike kurejea katika vyuo vikuu na kuhakikisha wanawake wana fursa ya kupata elimu katika ngazi zote.
Wiki hii ni maadhimisho ya mwaka ilisitisha wanawake kuhudhuria masomo katika taasisi za elimu ya juu za umma na binafsi, na kuifanya nchi maskini ya Afghanistan kuwa ni nchi pekee duniani kupiga marufuku kwa wasichana kupata elimu ya kuanzia darasa la saba na kuendelea.
Thomas West, mwakilishi maalum wa Marekani kwa Afghanistan, ameiita marufuku hiyo ya mwaka mzima katika elimu ya chuo kikuu “haina utetezi.”
Aliandika katika mtandao wa X, uliokuwa unajulikana kama Twitter, kuwa mgogoro unaolikumba taifa la Asia Kusini “linahitaji kizazi siku za usoni cha wanawake madaktari, wahandisi, viongozi wa biashara, na waalimu ili kukua na kufanikiwa na kujitegemea.”