Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani la WHO (IARC) inasema kuwa kupiga marufuku uuzaji wa tumbaku kwa watu waliozaliwa kati ya 2006 na 2010 kunaweza kuzuia karibu vifo milioni 1.2 kutokana na saratani ya mapafu kufikia mwisho wa karne hii, ulisema utafiti wa modeli uliotolewa Alhamisi.
Uvutaji sigara unasababisha takriban asilimia 85 ya visa vyote vya saratani ya mapafu, saratani mbaya zaidi ulimwenguni, kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni.
Ikiwa mwelekeo wa sasa utaendelea, kutakuwa na karibu vifo milioni tatu vya saratani ya mapafu kati ya watu waliozaliwa kuanzia 2006 hadi 2010, ulisema utafiti huo mpya kutoka (IARC).
Lakini kama mauzo ya tumbaku yangepigwa marufuku kwa watu hawa milioni 650, karibu vifo milioni 1.2 vinaweza kuzuiwa ifikapo mwaka 2095, ilikadiria utafiti wa kielelezo uliochapishwa katika jarida la Lancet Public Health.
Utafiti huo, moja ya tafiti za kwanza zilizolenga kutathmini athari za kizazi kisicho tumia bidhaa za tumbaku, ilipitia data kuhusu visa vya saratani na vifo kutoka nchi 185.
Zaidi ya asilimia 45 ya vifo vya saratani ya mapafu kati ya wanaume kote ulimwenguni vinaweza kuzuiwa, na karibu asilimia 31 kati ya wanawake, utafiti uligundua.