Usiku wa kuamkia October 31 2016 Tanzania ilimpoteza bondia maarufu wa ngumi za kulipwa Thomas Mashali ambapo ilielezwa kuwa Marehemu Mashali alifariki kwa kushambuliwa na watu baada ya kusingiziwa ni mwizi na watu ambao aligombana nao maeneo ya Kimara Dar es salaam.
Leo December 8 2016 kwa mara ya kwanza watuhumiwa saba wa mauaji ya bondia huyo wamefikishwa mahakama ya hakimu mkazi Kinondoni na kusomewa shitaka la mauaji, kesi hiyo itatajwa tena December 20 2016 na watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.
VIDEO: Polisi ilivyoongea kuhusu waliyomuua bondia Thomas Mashali, Bonyeza play hapa chini kutazama
AUDIO: Saa chache kabla ya kifo kumkuta Bondia Thomas Mashali, Bonyeza play hapa chini