Mashabiki wa Arsenal leo wameandamana nje ya uwanja wa Emirates kuelekea mchezo wao dhidi ya Everton wakipinga mmiliki wa timu hiyo Bilionea Stan Kroenke kwa kitendo chake cha kuruhusu Arsenal ishiriki European Super League michuano ambayo imepingwa na UEFA na FIFA.
Mtoto wa Kroenke anayejulikana kama Josh Kroenke atolea ufafanuzi sula hilo kwa niaba ya baba yake kuwa hawakuwa na nia ya kuiuza Arsenal.
“Hatuna nia ya kuiuza naamini tunatosha kuendelea kuiendesha Arsenal, tulikuwa katika hali ngumu ya kulazimishwa kutoka (Arsenal)”
Arsenal walikuwa miongoni mwa Club sita za England zilizokuwa zimeridhia kushiriki michuano mipya ya European Super League ambayo imekosolewa vikali kuwa na lengo la kutafuta pesa na sio kukuza soka.