Hospitali ya Ampola Tasakhtaa inayotoa huduma za matibabu ya urembo hapa nchini imemtambulisha Daktari Bingwa kutoka Egypt ambaye atahusika kutoa matibabu kwa watu wanaosumbuliwa na matatizo mbalimbali ya uzazi, sambamba na kumtambulisha Balozi wake mpya wa hospitali hiyo ambaye ni msanii Masha love.
Hospitali hii iliyopo Zanzibar inahusika katika utoaji wa huduma tofauti tofauti za urembo bila kuwa na madhara yeyote katika mwili wa binadamu kama vile Urembo wa kuongeza matiti na makalio, Urembo wa sura kwa kuongeza mashavu, midomo, kutoa mikunjo usoni, vinyama usoni na kutoa mafuta usoni.
Mbali na hivyo Hospitali ya Ampola Tasakhtaa inatoa pia huduma za Plastic surger, kuondoa mawe kwenye figo na kuotesha nywele kwa wenye vipara.