Kwa mujibu wa mashuhuda na watumishi wa afya, raia 40 waliuawa jana huko Nyala, mji mkuu wa Jimbo la Darfur, Kusini Magharibi ya Sudan, katika mashambulizi ya anga kwenye soko maarufu na vitongoji vya kiraia.
Habari zimesema kuwa ndege za kivita zilifanya mashambulizi makali zikilenga maeneo ya makazi, ikiwa ni pamoja na vitongoji vya Al-Sad Al-Ali, Al-Riyadh, na Texas, na soko maarufu la Al-Malaja huko Nyala.
Kituo cha afya cha Al-Wohda huko Nyala kilipokea idadi kubwa ya wagonjwa waliopatwa na kiwewe, ambapo baadhi yao walikufa njiani wakati wakikimbizwa kwenye kituo hicho, na wengine walikufa baada ya kuwasili, na kufanya idadi ya vifo kuweza kuongezeka zaidi.
Vikosi vya Msaada wa Haraka RSF vimesema kuwa msako bado unaendelea kutafuta miili iliyonasa chini ya vifusi.