Raia yeyote wa Ukraine sasa anaweza kutuma maombi ya uraia wa Urusi chini ya mpango uliorahisishwa, kulingana na amri iliyotiwa saini na Rais Vladimir Putin siku ya Jumatatu.
Hatua hiyo pia inatumika kwa watu wasio na utaifa wanaoishi kwa kudumu nchini Ukraine na pia kwa raia wa jamhuri mbili za Donbass, zilizotambuliwa hapo awali na Urusi kama Jamhuri huru.
Waukraine sasa wanaweza kuwasilisha ombi husika bila hitaji la kuishi Urusi kwa miaka mitano, kuwa na chanzo cha mapato au kufaulu mtihani wa lugha ya Kirusi – jambo ambalo kwa kawaida wageni wanatakiwa kufanya kabla ya kutuma ombi la uraia wa Urusi.