Mashindano ya Polisi Jamii Cup ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka maeneo tofauti tofauti hapa nchini ambapo yamekuwa yakiwakutanisha Jeshi la Polisi na jamii huku mashindao hayo yakitumika pia kuwakumbusha wananchi kushiriki katika chaguzi zijazo na Jeshi hilo kuwaomba wananchi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu katika Jamii.
Awali akiongea na washiriki wa mashindano hayo octoba 03,2024 jijini Arusha Kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo Nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Simon Pasua amesema imekuwa ni desturi ya Jeshi hilo kushirikisha jamii katika michezo ambapo alibainisha kuwa dhana hiyo imekuwa na matokea Chanya katika kuwakutanisha na Jeshi la Polisi.
Ameongeza kuwa mwaka huu na mwaka ujao ni miaka ya chaguzi kwa ngazi zote ambapo ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi kushiriki katika chaguzi hizo huku akiweka wazi kuwa Jeshi hilo pia litashiriki katika ulinzi, akiwataka kuendelea kutunza amani na kuwafichua wahalifu.
Fatuma Mwanga kutoka taasisi ya uhasibu Arusha yeye akajigamba kwa kuibuka na ushindi kwa magoli 28 kwa tisa dhidi ya wapinzani wao chuo cha ufundi Arusha ambapo alibainisha kuwa ushindi wao unatokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya kwa Pamoja na timu yake huku akiwataka wapinzani wao kujipanga tena katika mashindano yajayo akasisitiza kuwa mashindao hayo yamekuwa fursa pia ya kukutana na Jeshi la Polisi.
Askari wa kike kutoka katika kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo Makao Makuu akaweka wazi furaha yake katika mashindano hayo ambayo yamekuwa chachu ya kuwaweka karibu na jamii hususani jamii hiyo ya ambayo ni yakifugaji kutoka Mkoa wa Arusha.
Nae Karen Kabelinde ambaye ni mchezaji wa kutoka chuo cha ufundi Arusha akabainisha kuwa mchezo ulikuwa mzuri kwa timu zote mbili ambapo amesema kuwa wanajipanga kwa michezo ijayo kutokana na kupoteza mchezo huo huku akiomba mashindao kuendelea ili kuwa karibu zaidi na Jeshi hilo.