Vijana 11 wenye umri kati ya miaka 20 na 25 wakiwemo Mawakala wawili wa kusajili laini za simu, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mbeya kwa tuhuma za kuwatapeli wananchi wakitumia majina ya viongozi wa Serikali pamoja na wasanii maarufu nchini.
Aidha vijana hao wanadaiwa kuwa walikuwa wanatumia laini za simu ambazo zimesajiliwa kwa kutumia vitambulisho vya watu wengine, kuwatapeli wananchi kwa kuwatumia jumbe fupi za simu zinazosema ‘ile pesa itume kwenye namba hii’