Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2023 ambapo jumla ya Watahiniwa 104,549 sawa na asilimia 99.23 ya Watahiniwa waliofanya mtihani huo wamefaulu ambapo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 0.26 ikilinganishwa na mwaka jana.
Katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt. Said Mohamed ametangaza matokeo hayo leo Visiwani Zanzibar ambapo amesema mwaka 2022 Watahiniwa waliofaulu walikuwa ni 93,136 sawa na asilimia 98.97, hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 0.26 ikilinganishwa na mwaka 2022.
“Wanawake waliofaulu ni 46,707 sawa na asilimia 99.51 wakati Wanaume waliofaulu ni 57,842 sawa na asilimia 99.00”