Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania bara klabu ya Dar Es Salaam Young African September 13 wameshuka dimbani kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu dhidi ya klabu ya Coastal Union ya mkoani Tanga, mchezo umepigwa katika uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.
Mechi iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Yanga kuona usajili waliyofanya katika timu yao pamoja na kuangalia kuwa historia itajirudia kumfunga Coastal Union kwa idadi kubwa ya magoli kama msimu uliyomalizika? huku kwa upande wa Coastal Union wakiwa wamekamilika chini ya kocha wao Jackson Mayanja kutoka Uganda.
Mechi imemalizika kwa klabu ya Dar Es Salaam Young African kuibuka na ushindi wa goli 2-0, goli la kwanza likitiwa wavuni na Saimon Msuva dakika ya 8 ya mchezo, Donald Ngoma akifunga goli la pili kwa kutumia krosi safi kutoka kwa Saimon Msuva dakika ya 42 kipindi cha kwanza.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos