Ligi Kuu Hispania Laliga imeendelea tena leo October 31 kwa vilabu kadhaa kukipiga katika viwanja mbalimbali, Real Madrid ya Hispania walikuwa wenyeji dhidi ya Las Palmas katika dimba la Santiago Bernabeu kuwania point tatu muhimu ambazo zitasaidia kujiweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa Ligi Kuu.
Real Madrid ambayo ipo chini ya kocha Rafael Benitez lakini inahusishwa kwa kiasi kikubwa kutaka kumrudisha kocha Jose Mourinho ambaye amewahi kuitumikia klabu hiyo kwa miaka mitatu, wameibuka na ushindi wa jumla ya goli 3-1 na kuweza kupata point tatu muhimu kuelekea safari ya kuwani ubingwa wa Ligi Kuu Hispania.
Magoli ya Real Madrid yalifungwa na Isco dakika ya 4 ya mchezo ambapo Cristiano Ronaldo dakika 10 baadae akaongeza goli la pili, Las Palmas walipata goli la kwanza dakia ya 38 Hernan Santana, goli ambalo lilianza kufufua matumaini ya kusawazisha ila Real Madrid wakaongeza goli la tatu kupitia kwa Jese Rodriguez dakika ya 43, magoli ambayo yalidumu kwa dakika zote 90.
Video ya magoli ya Real Madrid Vs Las Palmas
https://youtu.be/rKJHKlwRdGs
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.