Moja ya headline ambazo zimechukua nafasi kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja na taarifa kwamba tafiti zinaonyesha kuwa mwanamke akinyonywa matiti na mwanaume inampunguzia kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa kansa, wengine wameenda mbali zaidi na kusema itafika time wanawake wataanza kuwalipa wanaume pesa ilitu wawasaidie kuwanyonya matiti.
Millardayo.com imempata Naibu Waziri wa Afya, ustawi wa jamii, jinsia, wazee na watoto Hamisi Kigwangalla ambaye anasema kuwa sio kweli na ni upotoshwaji unafanyika.
‘Tafiti za tiba ni mama kumnyonyesha mtoto wake kwa miezi 12 na zaidi wala sio huko wanakozungumzia kwenye mitandao, kitaalamu ukinyonyesha mtoto kwa zaidi ya miezi 12 unapunguza kiwango cha uambukizo wa saratani ya matiti kwa asilimia 64‘ –Waziri Kigwangalla
‘Nimeona watu wanasema kuna wakati wanawake watakuwa wakiwalipa wanaume ili wawanyonye matiti huo ni upotoshwaji, wanachotakiwa kukijua ni kufuata misingi ya malezi kwa watoto ikiwa ni pamoja na kuwanyonyesha watoto wao kwa wakati‘ –Waziri Kigwangalla
Unaweza kuendelea kumsikiliza Waziri Kigwangalla
ULIIKOSA HII YA WAZIRI MWIJAGE KUHUSU SUKARI YA BAKHRESA