Matumaini ya Barcelona kumsajili Joshua Kimmich yamepata pigo, huku Bayern Munich wakiwa tayari kuanza mazungumzo na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kuhusu kandarasi mpya, inaripoti Mundo Deportivo.
Kiungo huyo amekuwa akilengwa kwa muda mrefu na Barca, ingawa klabu hiyo ya Uhispania inasumbuliwa na masuala ya kifedha yanayoendelea.
Hata hivyo, mchezaji huyo akieleza waziwazi kukerwa kwake na bosi wa Bayern Thomas Tuchel, pamoja na jinsi msimu ulivyosonga mbele kwa Bayern huku mabingwa hao watetezi wakionekana kuwa na uwezekano wa kumaliza nafasi ya pili kwa Bayer Leverkusen minong’ono ya kuondoka kwa Kimmich ilikuwa ilizidishwa.
Hata hivyo, meneja mpya wa michezo wa Bayern Max Eberl anaamini kuwa hali kati ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani na klabu hiyo itaimarika sasa baada ya Bayern kuthibitisha kwamba Tuchel ataondoka mwishoni mwa msimu huu.
Kimmich, ambaye mkataba wake unamalizika 2025, pia amekuwa akihusishwa na Manchester City na Manchester United.