Matumizi ya teknolojia wakati wa usikilizwaji wa mashauri kwenye Mahakama nchini kumetajwa kupunguza malalamiko ya vitendo vya rushwa na urahisishaji wa upatikanaji haki kwa wakati.
Hayo yamebanishwa na Dokta Angelo Rumisha Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania na Mkuu wa kitengo cha maboresho ya mahakama nchini wakati akizungunza na Waandishi wa habari kituo jumuishi Cha utoaji haki Morogoro ambapo amesema kabla ya kuanza kwa matumizi ya teknolojia kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi Kuhusu changamoto upatikanaji wa haki.
Rumisha anasema licha ya kupunguza malalamiko kwa wananchi pia imerahisisha ufanyaji kazi kwa mahakimu na majaji wa kuahirishwa kwa mashuuri mara kwa mara .
“Sasa hivi kesi zote zinasajiliwa mitandaoni mlalamikaji anaweza kusajili hata saa nane Usiku mtandaoni ikakupa maelekezo na kupagiwa hakimu au jaji wa kusikiliza bila kupitia Kwa karani”
Amesema suala la utoaji haki linapande nyingi ikiwemo ushahidi hivyo jamii inatakiwa kufahamu umuhimu wa kuhudhuria kwenye mashauri kutoa ushahidi kwenye kesi Ili haki iweze kupatikana kwa wakati.
Nao baadhi ya wananchi mkoani Morogoro wamesema kwa sasa jamii imekua na imani na mahakama kutokana na masuala mbalimbali kuwa na uwazi ikiwemo utolewaji wa nakala za hukumu kwa lugha ya kiswahili.