Mauricio Pochettino ameyazima mazungumzo ya Chelsea ya kutaka kumnunua Kylian Mbappe.
The Blues inasemekana kuwa moja ya vilabu kadhaa vya Premier League vinavyotarajia kumshawishi supastaa huyo wa Ufaransa kwenye mchezo wa Uingereza huku PSG ikiwa tayari kumuuza mshindi huyo wa Kombe la Dunia.
Lakini kocha mpya wa Chelsea, Pochettino, amekiri mapenzi yake kwa mchezaji wake wa zamani wa PSG, MBappe, alisema:
“Tunafanyia kazi ukweli wetu, ukweli wetu ni tofauti. “Kwa upande wangu, hakuna cha kusema. Natumai tu watapata suluhisho kwa pande zote mbili. “Naipenda PSG, nilikuwa mchezaji na kocha pale … na ninampenda Kylian”.
Pochettino aliwahi kufanya kazi na Mbappe wakati alipokuwa meneja wa PSG, na amekiri kufanya hivyo.
“Tunafanyia kazi ukweli wetu, kwani ukweli wetu ni tofauti. Kwa upande wangu, hakuna cha kusema, ni kuwaunga mkono tu. Natumai watapata suluhu kwa pande zote mbili. Ni klabu ninayoipenda kwa sababu nilikuwa mchezaji, nahodha na kocha. Pamoja na Kylian tuliunda uhusiano mzuri sana, natumai wanaweza kupata suluhisho bora kwa pande zote mbili.”
Mabingwa hao wa Ligue 1 wamemuacha Mbappe kwenye kikosi chao cha kujiandaa na msimu ujao nchini Japan huku kukiwa na hofu kwamba tayari ana makubaliano na Real Madrid kujiunga bila malipo mwaka 2024.