Mauzo ya magari yanayotumia umeme yafikia 54% ya mauzo ya magari yote mapya huko nchini Norway, ikiwa ni mara ya kwanza kwa nchi hiyo kurekodi mauzo ya juu ya magari hayo dhidi ya yale yatumiayo Dizeli na Petroli.
Serikali ya Norway ina mpango wa kukataza mauzo ya magari yatumiayo Petroli na Dizeli ifikapo mwaka 2025, ambapo tayari imeanza mikakati ya kupunguza kodi ili kuhamasisha utengenezwaji wa magari ya umeme kwa wingi.
Kwa mwaka 2020 mauzo ya magari ya umeme yamefikia 54% ya magari yote mapya ya abiria, ikiwa ni ongezeko la kutoka 49% mwaka 2019.
Hata hivyo, mwezi Desemba umerekodi mauzo ya juu zaidi ya magari kwani zaidi ya magari mapya 20,000 yalisajiliwa, ambapo 66%.7 yalikuwa magari yatumiayo umeme na yapatayo 4,232 yalikuwa ni aina ya Tesla Model 3, ikiwa ni zaidi ya 20% ya mauzo yote ya magari kwa mwezi huo.