Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Silaa ameitaka Serikali kuweka Utaratibu mzuri wa kufanya uthamini na kulipa Wananchi kwa wakati akisisitiza lazima Fedha ziwe zimeshatengwa wakati uthamini unafanyika.
Wakati wa Majadiliano ya Bajeti ya Wizara ya Ardhi, amesema “Mara nyingi uthamini unafanyika lakini Taasisi inaagiza hivyo hata Fedha kwenye Bajeti haijatengewa. Matokeo yake Fidia zinachelewa na Wananchi wanapata shida”.
“MAWAZIRI NI MARUFUKU KUNYANYASA WATU, KUNA WENGINE MABINGWA KUWEKA WATU NDANI”-JERRY SILAA