Wananchi wa Liberia wanasubiria kwa hamu tukio la kuapishwa kwa Rais mteule George Weah, ambapo wengi wamekesha katika uwanja wa mpira wa taifa hilo, mahali ambapo leo January 22, 2018 anategemea kuapishwa na kuandika historia mpya kutoka kung’aa kwenye soka hadi kuwa Rais
George Weah, maisha yake ya utoto, yalikuwa katika mazingira duni katika mji mkuu wa Liberia Monrovia, alipata mafanikio makubwa katika soka na kufanikiwa kuchezea timu kadhaa barani Ulaya ikiwemo Chelsea, Monaco na AC milan.
Ni Muafrika pekee kuwahi kushinda tuzo mchezaji bora wa FIFA na tuzo ya Ballon. Weah aliingia katika siasa baada ya kustaafu soka mwaka 2002 na akawa miongoni mwa Maseneter katika bunge la Liberia.
Aligombea urais mwaka 2005 na alimshinda Johnson Sirleaf wakati wa duru ya kwanza katika uchaguzi huo lakini akashindwa katika duru ya pili ambapo kambi yake ilisusia kushiriki.
Aliyewahi kuwa meneja wa George Weah katika klabu ya Monaco ya ligi kuu ya Ufaransa Arsene Wenger amealikwa na atakuwepo katika tukio la kuapishwa.
GOLI LA YANGA VPL LILILOPATIKANA BAADA YA KUCHEZA DAKIKA 225 BILA KUFUNGA