Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Anatropia Theonest amelazimika kukaa maskani ili kuzungumza na wananchi wa maeneo ya Tabata Kimanga kwa lengo la kubaini changamoto zinazowakabili.
Moja ya maskani aliyokaa mbunge huyo alijikuta akinywa Kahawa ili kusikiliza changamoto ambapo alilalamikiwa na wananchi kuhusu ubovu wa miundombinu ya barabara za mitaa ambazo asilimia kubwa hazipitiki na kuwa mithili ya mito.
Juma Kijuu ni mmoja wa wakazi wa maeneo hayo ambapo amesema “Hali harisi ya mazingira yetu yanaonekana kwani ni kilio cha muda mrefu, hii ni barabara lakini ukiangalia imekuwa kama mto, hivyo tunashukuru umefika,”.
Mbunge huyo amesema kuwa changamoto hizo ameziona, hivyo anaongeza kasi ya kupigia kelele suala hilo ili liweze kutatuliwa kwa haraka.