Mazishi makubwa yalifanyika Jumatano huko Kivu Kaskazini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa wahasiriwa wa ajali ya feri iliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 78.
Mazishi hayo yaliyofanyika katika makaburi ya Makao ya Nyiragongo ilihudhuriwa na viongozi kutoka sekta mbalimbali na wawakilishi wa makundi ya kiraia na kuongozwa na mawaziri wa mambo ya ndani na masuala ya kijamii.
Mapema Jumatano, familia zilialikwa kutembelea vyumba vya kuhifadhia maiti huko Goma ili kupata habari kuhusu waliopotea
Familia hizo bado zinakabiliwa na sintofahamu huku wengi wao wakiwa hawajulikani waliko.
Mamlaka zimesema shughuli za utafutaji zinaendelea, lakini zimezitaka familia kutokuwa na wasiwasi kwa sababu ya uwezekano mdogo wa kupata manusura