Chombo cha habari cha Iran, Tasnim, ambacho kina mfungamano na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini humo, kinaripoti kuwa mazishi ya Rais Ebrahim Raisi yatafanyika kesho Tabriz – mji aliokuwa akisafiria jana.
Kituo hicho kinasema mazishi ya watu wengine wote waliofariki pia yatafanyika, ikinukuu kauli ya maafisa katika jimbo la Azerbaijan Mashariki mwa Iran.
Miili hiyo kwanza itapelekwa kwa idara ya uchunguzi wa kitaalamu huko Tabriz.
Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei pia ametoa taarifa rasmi na kutangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa kwa heshima ya rais Raisi.
Wakati huo huo Baraza la mawaziri la Iran limemteua Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Ali Bagheri Kani kuwa kaimu waziri wa mambo ya nje, kufuatia kifo cha Hossein Amir-Abdollahian, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.