Mazungumzo ya kuwaachilia mateka 239 wanaoshikiliwa na Hamas yamekwama baada ya kundi la wanamgambo kuitaka Israel kuruhusu usafirishaji wa mafuta Gaza, afisa wa zamani wa Marekani mwenye ujuzi wa mazungumzo hayo ameiambia tovuti mshirika wetu NBC News.
“Hamas imekuwa ikisisitiza kupokea mafuta,” walisema.
“Upande wa Israel na Marekani, pamoja na nchi nyingine, wanataka kundi kubwa la raia wao kuachiliwa huru.”
Afisa huyo wa zamani aliomba asitajwe jina kwa vile hawajaidhinishwa kuzungumza hadharani.
Afisa huyo wa zamani wa Marekani, afisa wa Israel na mwanadiplomasia mwenye ujuzi wa mazungumzo hayo, alisema majadiliano yalivunjika kabla ya Israel kuanzisha awamu ya pili ya mashambulizi yake Ijumaa jioni na kutuma wanajeshi wa ardhini huko Gaza.
Mateka hao wanaaminika kuwa ni pamoja na watu walio na hati za kusafiria kutoka nchi 25 za kigeni, wakiwemo raia wanaokadiriwa kufikia 54, Waajentina 15, Wamarekani 12, Wajerumani 12, Wafaransa sita na Warusi sita.
Mazungumzo ya awali, yaliyopatanishwa na Qatar, yalisababisha kuachiliwa kwa mateka wanne, Wamarekani wawili na wanawake wawili wazee, kwa siku mbili tofauti.