Siku ya tano baada ya majeshi ya Urusi kuingia Ukraine, wajumbe kutoka nchi hizo mbili wameanza mazungumzo yenye lengo la kumaliza vita.
Ofisi ya rais wa Ukraine inasema inataka kusitishwa mara moja kwa mapigano na kuondolewa kwa vikosi vya Urusi.
Wakati huo huo Moscow inataka kufikia makubaliano ambayo yalikuwa kwa maslahi ya pande zote mbili, kulingana na mpatanishi wa Urusi, Vladimir Medinsky.
Kabla ya mkutano huo kuanza, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliwataka wanajeshi wa Urusi kuweka chini silaha zao, na kutoa wito kwa EU kuipatia Ukraine uanachama wa umoja huo mara moja