Aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini ambaye kwasasa ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijni Prof.Sospeter Mwijarubi Muhongo ametaja vyanzo vipya vya uhakika vinavyoweza kuondoa tatizo la upungufu wa Umeme nchini.
Prof. Muhongo akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya Nishati kwa mwka wa fedha 2024/25 amevitaja vyanzo hivyo kuwa ni Umeme wa jua,Umeme wa Upepo na Umeme unaotokana na joto ardhi ambao nchi Jirani ya Kenya imefanikiwa kuzalisha umeme huo kwa kiwango kikubwa.
“Nawathibitishia vyanzo vya uhakika kuwa jua linavyopiga ardhini ‘square meter’ moja unapata bulb tatu au nne za umeme yaani ni waltz 342 nataka kuwaonesha kwanini Tanzania tunatakiwa kwenda huko sasahivi nah ii sisemi msiache mengine nachukulia mfano wa India na China kwasasa hivi sola ni Giga waltz 82 na hii zodisha mara 1000 upate Mega waltz na aina ya pili ni upepo na upepo ambao unaweza kuzalisha umeme lazima speed yake iwe mita nne kwa sekunde ikiwa 50 au 60 kama speed ya gari uzalishaji unakuwa ni mkubwa sana kwa Afrika tujifunze kwa wenzetu wakenya wao wao wanaumeme mwingi Zaidi wanaongoza kwa Afrika wana Mega waltz 440” Prof. Muhongo