Kylian Mbappé ameendelea na msimamo wake mkali dhidi ya Paris Saint-Germain (PSG) kwa kukataa Ofa ya upatanishi katika mgogoro wa kifedha wa thamani ya euro milioni 55 (dola milioni 60).
Mshindi huyo wa Kombe la Dunia na Nyota wa Ufaransa alikataa ombi la upatanishi la tume ya kisheria ya Ligi ya Soka ya Ufaransa siku ya Jumatano katika mzozo wake na klabu yake hiyo ya zamani kuhusu mishahara na bonasi.
Nyota huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa, ambaye sasa anachezea Real Madrid, amedai kuwa PSG anaidai mshahara wa miezi mitatu na sehemu ya bonasi ya uaminifu.
Aidha PSG, kwa upande wake, imedai kuwa Mbappé alikubaliana kutokulipwa bonasi hizo baada ya kutoongeza mkataba wake na kuondoka klabuni bila malipo, hata hivyo, wawakilishi wa Mbappé wamekanusha madai hayo, wakisema hakuna makubaliano ya siri yaliyowahi kufanyika.
Klabu ya PSG imependekeza suluhisho kupitia upatanishi, lakini Mbappé ameonyesha wazi kuwa hatua hiyo haitakuwa na maana na ikiwa mgogoro huu hautapatiwa suluhisho, kesi hii huenda ikaishia mahakamani.