Real Madrid iko tayari kutoa pauni milioni 200 kumsajili Kylian Mbappe bila kufanya mazungumzo na Paris Saint-Germain, kwa mujibu wa talk SPORT.
Vilabu vyote viwili havikufanya mazungumzo msimu huu wa joto licha ya Mbappe kufungiwa na mabingwa hao wa Ligue 1.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amerejea kwenye kikosi cha kwanza na amefunga mabao matano katika mechi zake tatu za kwanza za msimu huu.
Ingawa kuna uvumi kwamba Mbappe anaweza kuafiki mkataba mpya na PSG, inaaminika Real Madrid inakusudia kufikia makubaliano ya awali ya mkataba na mchezaji huyo mwezi Januari.
Hii itamaanisha kuwa nahodha huyo wa Ufaransa atajiunga nao bila malipo mkataba wake wa PSG utakapokamilika Juni 30.
Real hawakupenda rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi kukataa mbinu zao, hata ofa zinazokaribia pauni milioni 172.
Badala yake, Real wameamua kutenga karibu pauni milioni 200 kwa Mbappe kama mshahara na ada ya kusaini.