Nyota wa Ufaransa, Kylian Mbappe alielezea furaha yake kwa ushindi ambao timu hiyo iliupata jana dhidi ya Beets 2-0 katika mzunguko wa nne wa La Liga na kuzungumzia namna ambavyo watu wanadai yeye ni mrithi wa Christiano Ronaldo.
Mbappe, mfungaji wa mabao hayo mawili, alisema: “Mrithi wa Cristiano.” “Hapana, yeye ni mfano wangu, lakini hapana, sitaki shinikizo hili. Nataka kuwa Kylian. Shinikizo pekee ninalokabiliana nalo ni kuzoea timu.”
Aliongeza. “Naweza kucheza katika nafasi zote tatu za ushambuliaji.”
Na kuhusu kufunga mabao mawili: “Nilijua wakati huu unakuja. Bao langu la kwanza lilimwendea Fede Valverde.”
Aliongeza kuhusu kupiga mikwaju ya penalti kati yake na Vinicius: “Kocha anasema tutapiga mikwaju ya penalti pamoja? Sitaki kulazimisha mambo, haya sio mawazo yangu.”
Alimalizia hivi: “Ukosoaji? sishangai. Ni sehemu ya maisha. nimezoea.”