Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Zuberi Habibu mkazi wa Kijiji cha Madudumizi B kata ya Zombo Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro anashikiliwa kwa vyombo vya ulinzi na usalama Wilayani humo kwa tuhuma za mauaji ya Watu wawili na kumjeruhi mmoja.
Mwenyekiti wa kamati ya usalama Wilaya ya Kilosa ambaye ndio mkuu wa Wilaya hiyo shaka Hamdu Shaka amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku chanzo kikitajwa kuwa mtuhumiwa hakutaka baba yake mzazi kukodisha mashamba kwa watu wengine
Dc shaka amesema waliouawa kwenye tukio hilo ni Habibu Liomite ambaye ni Baba mzazi wa Mtuhumiwa , Hasani Khalid mjumbe wa serikali ya mtaa huku Hamisi Msabaha ambaye ni mwenyekiti wa Kijiji akijeruhiwa.
Amesema tayari Mtuhumiwa ameshakamtwa kusubriri taratibu zingine za kisheria.