Kwenye watu wazito walioamua kuingia kwenye siasa, mfanyabiashara Yusuph Manji pamoja na Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe, Mkubwa Fella ambaye ni Diwani wa kata ya Kilungule nao waliamua kuthubutu upande huu wa pili wa siasa.
Leo December 31 2015 Diwani Manji alikutana na watu wake wa Mbagala kwa ajili ya kuwashukuru kabla haujaisha mwaka 2015 kwa nafasi waliyompa kuwatumikia pamoja na kuwaahidi kufanya kazi kwa bidii na pia kutowaangusha mpaka atakapofikia mwisho wa udiwani wake kwa heshima.
Kwenye mwaliko huo kulikuwa na Madiwani pia kutoka Kata mbalimbali za Temeke na maeneo mengine walioungana nae pia.
Kulikuwa na burudani pia ya wasanii mbalimbali walioalikwa kwenye sherehe hiyo.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE