Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali haiongozi kibabe na lengo ni kulifanya Taifa liwe salama kwani Watanzania wanahitaji maendeleo na hakuna Mbunge au Diwani aliyezuiliwa kufanya mikutano kwenye maeneo yake.
Ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Freeman Mbowe aliyehoji ”Ni lini Serikali itaruhusu vyama vya siasa vifanye wajibu wake wa uenezi ili kujiandaa na Uchaguzi Mkuu na Serikali ina mpango gani wa kuwezesha Taifa kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi ili uchaguzi uwe wa haki na halali”.
Waziri Mkuu amesema Vyama vya siasa havijazuiliwa kufanya shughuli zake ila umewekwa utaratibu muhimu kwa viongozi waliopata ridhaa kwenye maeneo yao na ratiba za uchaguzi zitatolewa na kueleza lini shughuli za kampeni zitaanza.
HISTORIA: DANIEL ARAP MOI JABARI LA SIASA AFRIKA, JASUSI ALIEPINDULIWA, UFISADI