Wadhamini wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, wameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wamemwandikia barua Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ya kumuomba awasaidie kumleta Mshitakiwa Tundu Lissu nchini .
“Wakati tunamdhamini Lissu hatukujua kama atapigwa risasi na kuondoka, tumemuandikia barua Mbowe ili atusaidie kumleta Tanzania na sisi tuweze kumleta Mahakamani, tunaomba muda zaidi wa kufuatilia majibu ya barua hiyo”– Katula, Mdhamini wa Tundu Lissu.
“Tunaomba mtuletee Mshtakiwa hapa, tena (Mdhamini) usije ukafikiri tutakusamehe tunakupa muda mwingine tuletee Mtu huyo kabla hatujatoa amri nyingine itakayokuwa ngumu zaidi dhidi yenu Wadhamini na Mshitakiwa (Lissu) mwenyewe, naahirisha kesi hadi Februari 20, 2020″-Hakimu Simba
MAOMBI YA UMILIKI WA SILAHA YAMSHTUA RC KILIMANJARO, WAMO VIONGOZI WA DINI