Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeutaka upande wa mashtaka kuhakikisha wanakamilisha upelelezi katika kesi ya kughushi na utakatishaji fedha inayomkabili aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Michael Wambura.
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina, aliyasema hayo baada ya upande wa mashtaka kudai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na kwamba kuna maeneo machache ya kukamilisha upelelezi.
Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, alidai kesi hiuo lilipelekwa kwa kutajwa na kuna maeneo machache ya kukamilisha upelelezi hivyo, aliomba tarehe nyingine kwa kutajwa.
Wakili wa utetezi Nestory Wandiba, alidai upande wa mashitaka umekuwa ukieleza maneno matamu lakini hayazai matunda hivyo, wanatakiwa kuangalia athari ambazo anazipata mshitakiwa.
Hakimu Mhina, aliutaka upande wa jamhuri kuhakikisha upelelezi unakamilika na aliahirisha kesi hiyo hadi Agusti 21, mwaka huu.
FAHAMU IDADI YA SAMAKI WALIOPO TANZANIA