Zaidi ya Wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama Machinga (90) wanaofanya shughuli zao pembezoni mwa soko kuu wa Chifu Kingalu Manispaa ya Morogoro wametakiwa kuhama katika vibanda hivyo kwa madai kuwa vipo katika eneo sio rasmi.
Akizungumz na Ayo tv na Millard ayo .com mmoja wa wafanyabiashara aliyejiatumbullisha kwa jina Hamis Hamza amesema disemba 5 mwaka huu wamepewa barua za kuhama katika eneo hilo na kutakiwa kuhamia eneo la nyuma ya soko jambo ambalo wao wanaona linawapa changamoto hasa kupata wateja.
Wanasema licha ya eneo hilo kutokuwa rafiki Kwa wateja lakini pia tayari vibanda hivyo waligaiwa watu wengine hivyo hofu Yao kuingia migogoro na wafanyabiashara wengine.
Kutoka na changamoto hiyo ikamlazimu Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Abdu lazaz Abood amefika katika soko hilo na kuzungunza na wafanyabiashara hao.
Mhe. Abood amesema ni lazima Serikali kabla ya kuwaondoa itenge eneo Maalum ambalo litakuwa rafiki kwaoili waweze kufanya biashara kama kawaida bila kuathiri mitaji yao.
Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan anapenda vijana kujiajiri hivyo yeye kama Mbunge hatukubali suala hilo kwani wengi wao wanekupa fedha za asilimia Kumi NJ lazima wawekewe mazingira rafiki.
Akitolea ufafanuzi suala hilo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Manispaaa ya Morogoro Lilian Heneriko amekiri wafanyabiashara hao kupewa notisi ya kuhama katika eneo hilo Ili kipisha ujenzi wa uzio na miundombinu mingine ya kiusalama.
Amesema eneo hilo linamachinga 500 hivyo wataondolewa ni 94 tuu na watahamishiwa eneo la nyuma ya soko sio watahamishiwa moja Kwa Moja.