Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe.Dokta Abdulaziz Abood ametoa milioni mbili Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Karoli Lwanga kata ya Mindu Manispaa ya Morogoro ambapo amesema Serikali ipo pamoja na viongozi wa dini na kutambua mchango wao katika suala la kudumisha amani.
Dkt. Abood ameyasema hayo wakati alipohudhuria harambee ya kuchangia vifaa vya muziki katika kanisa hilo la Parokia ya Mtakatifu Karoli Lwanga Kata ya Mindu Manispaa ya Morogoro ambapo Mhe.Mbunge ametoa Shilingi Milioni mbili kwa ajili ya ununuzi Vifaa hivyo vya muziki ikiwa ni jitihada za kuunga mkono Viongozi dini na kutambua mchango wa waumini wa dini na kanisa hilo.
Dkt.Abood amesema Serikali inatambua mchango wa viongozi wa dini hivyo wataendelea kushirikiana katika masuala mbalimbali maendeleo Ili kuwasaidia wananachi.
Aidha Mhe.Abood amemshukuri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujali wananchi Kwenye sekta ya afya ambapo hivi karibuni ametoa magari ya kubeba wagonjwa.