Serikali imeingilia kati malalamiko ya Wananchi kukuhusu bando kuisha mapema maeneo ambayo yana huduma ya 5G kwa kuagiza TCRA kwenda kuangalia na kufanyia kazi changamoto hiyo kwa mujibu wa Sheria.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew wakati akijibu swali la Mbunge wa Msalala (CCM), Iddi Kassim leo Jumatatu, Novemba 6, 2023.