Leo September 8, 2020 Mbunge Johanna Ng’eno amekamatwa kufuatia matamshi aliyotoa dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta wikiendi iliyopita ambayo yanadaiwa kuwa ni maneno ya kumdhalilisha Rais huyo wa Kenya.
Video inayomuonesha Mbunge huyo akizungumzia mgogoro kati ya Rais Kenyata na Naibu wake, William Ruto imezua gumzo katika mitandao ya kijamii ambapo anasikika akimwambia Rais avunje Serikali ikiwa ameshindwa kufanya kazi na Ruto.
Baada ya kukamatwa kwa Ng’eno, Naibu wa Rais aliandika ujumbe katika Twitter yake akisema “viongozi wanapaswa kujizuia na kuepuka kutumia lugha ya matusi dhidi ya Wakenya wengine”.