Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimepokea kwa masikitiko barua ya kujiuzulu kwa Mbunge Mteule wa CCM Jimbo la Konde Sheha Mpeka Faki August 02, 2021.
Sasa millardayo.com imefanikiwa kumpata Mbunge huyo na kueleza sababu za kujiuzulu kwake…>>>Rasmi nimeamua kujiuzulu katika nafasi niliyopewa na Wananchi wa jimbo la Konde na maelezo niliyaandika yote katika ile barua”- Faki
“Tatizo nina changamoto za kifamilia ambazo zimenikwaza kutokutekeleza majukumu ya kibunge na kuwatumikia Wananchi wangu nimefanya hili binafsi ni maamuzi yangu mwenyewe wala sijashawishiwa na mtu yoyote najua kuna maneno watu wataongea lakini haya ni maamuzi yangu binafsi”- Faki