Mbunge wa Kahama Mjini kupitia CCM Jumanne Kishimba, ameiomba Serikali ifungue chuo cha wizi kwa kuwa matukio ya wizi katika sekta za umma na Halmashauri nyingi umeshamiri kwa kiasi kikubwa na kwamba chuo hicho kitasaidia wale watu wanaoenda kuchunguza wezi, kuzijua mbinu zao na kuwabaini.
Hayo ameyabainisha Jijini Dodoma wakati wa mkutano wa 19, kikao cha 39, wakati wa uchangiaji wa hoja ya Kamati ya Kudumu ya Huduma za Serikali za Mitaa, na kueleza kuwa ni vyema chuo hicho kikawekwa japo kwa kutumia jina lingine ili kukomesha suala hilo.
“CAG na Waziri wa Fedha yuko hapa hawa vijana wanaoajiriwa lazima wanatoka shule inayofundisha maadili mema na uaminifu, sasa wanaenda kupambana na wizi wengine wamesoma Seminari, kwanini serikali haifikirii sasa kuanzisha chuo cha wizi” Kishimba
“Kwa maana mtu anapochaguliwa kwa sifa ya uaminifu kwenda kupambana na wezi anaenda kupambana nao namna gani? afadhali apite kwenye chuo hicho kwa miezi mitatu ili ajue akili ya wizi, hawa vijana wetu tutawamalizia magerezani na hali ya wizi ni mbaya sana” Mbunge Kishimba
MWANRI AWEKA MASHARTI WANAFUNZI KUPIMWA CORONA NA MIMBA “MSIAZIMANE BARAKOA, MUWEKE NA LEBO”