Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani ameiomba Wizara ya Nichati kupitia kwa Waziri Dotto Biteko kuwezesha kupatikana kwa huduma ya umeme katika vijiji 26 vilivyosalia katika jimbo la ushetu ili kuwawezesha wananchi waishio katika maeneo hayo kutekeleza shughuli za kiuchumi na biashara.
Mheshimiwa Cherehani ameyasema hayo wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Nishati hii leo Bungeni jijini Dodoma ambapo amesema kuwa —— “tuna vijiji 112 kati ya hivyo 86 vina umeme na 26 havijapata umeme, kuna vijiji viwili vimesahaulika havijaingizwa kabisa kwenye mpango, kijiji cha Kalama na kijiji cha Nkale hivyo naomba vijiji hivi viweze kuwekwa kwenye mradi”.
Mhe. Cherehani ameomba pia Wizara ya Nishati kuwezesha kupatikana kwa mkoa wa Tanesco katika Mkoa wa Kahama ili kuwezesha uboreshwa kwa huduma ya umeme katika mkoa huo.
“Tunaomba Mkoa kwasababu hata katika Manispaa ya Kahama tu, makusanyo yake katika hoteli, viwanda na biashara zilizosajiliwa hivyo ni eneo linalohitajika kuangaliwa kwa macho ili kuepuka kukatika kwa umeme mara kwa mara” amesema Mbunge Cherehani.