Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Jesca Msambatavangu amesema Watanzania wanayo dhamana kubwa ya kuilinda nchi yao dhidi ya watu wenye nia ovu ya kuvuruga mila na desturi zilizopo, huku akibainisha kuwa wakina mama wanalo jukumu kubwa la kulea watoto katika maadili mema.
Mbunge Jesca ametoa kauli hiyo, wakati akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Mbogwe Mkoani geita katika ziara ambayo ameambatana na Mbunge wa jimbo la Mvumi Mkoani Dodoma Livingstone Lusinde (Kibajaji) wakiongozwa na Mwenyeji wao Nicodemus Maganga.
Jesca amewataka akina Mama wasiruhusu Mazingira ya Watoto kubwakwa na kufanyiwa vitendo vya ulawiti, huku Mbunge Lusinde akiwaomba wananchi kujenga misingi ya kuheshimu watendaji wa serikali.
Akizungumzia Maendeleo katika Jimbo la Mbogwe, Mbunge Maganga amesema katika Kipindi cha Mwaka wa fedha 2022/23 Halmashauri ya Mbogwe imeweza kukusanya zaidi ya Sh. Bilioni 25.
Katika hatua nyingine Mbunge Maganga amewaomba wabunge Jesca Mtambasavangu na Livingstone Lusinde kumuunga mkono Mbungeni wakati akitetea maendeleo ya Jimbo la mbogwe ambalo linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo miundombinu ya barabara, maji pamoja na huduma za nishati ya umeme.
Naye Mjumbe wa CCM Halmashauri ya Taifa Livingstone Lusinde amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na Mbunge Maganga kwani kwani ndio kwanza ameingia katika kuwahudumia wananchi na kuwaomba kuendelea kumuamini katika kipindi chote cha Mda wa Miaka Mitano ili aweze kutekeleza yale yote ambayo aliahidi kuyatekeleza.
Lusinde pia amewahasa wananchi wa Jimbo hilo kuhakikisha Maadili yanaendelea katika Familia zao huku akiwataka wananchi pia kuendelea kuheshimiana na Viongozi wa serikali pale ambapo kuna changamoto zinapelekwa sehemu husika na sio kuanzisha ugomvi usiokuwa na Tija kwa wanambogwe.