Mbunge wa viti maalum Jesca Kishoa akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2021/2022 iliyowasilishwa Bungeni leo June 2, 2021 na Waziri Dr. Medard Kalemani.
“Suala la mkataba wa SONGAS nimelizungumza mara nyingi sana, tumebakiza miaka miwili tu ili mkata huu uweze kuendelezwa, nina taarifa watu wa SONGAS wameshaanza kufanya ushawishi hadi kwa Wabunge kutaka mkataba wao uendeleekuwepo. Ninaomba Bunge tuupinge mkabata huu kama haujapitiwa upya kwasababu kama taifa hatunufaiki kwa namna yoyote”-Jesca Kishoa
“Masuala haya yameanza kuzungumza toka mwaka 2009 na CAG, Mheshimiwa Spika tunapoteza kila mwezi zaidi ya Dollar million tano kwasababu ya mkataba huu mbovu, Meshimiwa Spika nakuomba wewe pamoja na Mheshimiwa Rais tuupinge mkataba huu kwa ajili ya Wananchi”-Jesca Kishoa