Katika kukabiliana na adha ya wanafunzi wa kutembelea umbali wa zaidi ya km 12 mbunge wa jimbo la korogwe vijiji Timotheo Mnzava amekabidhi mabati 100,saruji mifuko 100 pamoja na tofalu 1500 kwaajili ya kuanzisha ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika kata ya magoma.
Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha kwamazandu kata ya magoma Mbunge mnzava alisema kuwa amekuwa akikutana na wanafunzi wakiwa wanatembea umbali mrefu kwenda shule pamoja na kurudi jambo ambalo linapelekea wanafunzi wengi hususa wakike kukutana na changamoto mbalimbali zinazopelekea baadhi yao kukatisha masomo.
“shule ya kwamazandu pamoja na makorora zina idadi kubwa ya wanafunzi idadi ya wanafunzi makorora peke yake kuna wanafunzi zaidia ya 60 wanafaulu kwenda shule ya sekondari na kwemanzandu pekea nako kuna idadi hiyo ya wanafunzi kila mwaka wanafaulu hivyo kwa shule zote mbili kuna zaidi ya wanafunzi miamoja hivyo wanatosha kuanzisha shule nyengine ya sekondari kwenye kata hii kwa upande huu kuwasaidia watoto wetu”
“kwasababu mara nyingi nikisema vitu wenzangu mnaniitikia na utekelezaji mzito leo nikasema siji na maneno matupu nafanya vitendo hiyo gari ninayo sema ina mizigo inakuja na tofali 1500 kwaajili ya kuanza ujenzi wa shule ya sekondari mpya tunafanya hivyo kwasababu tukisema maneno kila siku wanapiga piga chenga nime mwambia diwani leo nitafutie mchanga na mawe shuhulinyengine niachie mimi Alisema”mbunge.
Hata hivyo mbunge huyo amesema kuwa lengo ni kuhakikisha wajenga shule ya sekondari kwenye kata hiyo ya kisasa ili kusaidia wanafunzi wa shule hizo mbili za msingi kuweza kupata shule ya sekondari na hivyo malengo yao ni kukamilisha shule hiyo inakamilika mapema mwaka 2025 na hicyo kuwasaidia watoto hao kuweza kupata elimu yao kwenye mazingira ya karibu.