Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa, Mhe. Juliana Didas Masaburi katika kipindi cha Maswali na Majibu Bungeni Jijini Dodoma amehoji kuhusu uendeshaji wa Consolidators na De-Consolidators wanahusika katika kusafirishaji mizigo ya Wafanyabiashara.
Mbunge huyu amehoji na kusema kumekuwa na sintofahamu juu ya Wafanyabiashara pindi mizigo yao inapowasili nchini na kutokuwa na kumbukumbu ya risiti zao za awali.
‘Asante Mheshimiwa Mwenyekiti kwanza niungane na wenzangu kutoa Pongezi zangu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mwigulu kiukweli wote mnastahili Maua yao’- Julie
‘Mheshimiwa Mwenyekiti ningependa kuchangia kwenye mambo matatu kwanza Cargo Consolidation na De-Cosolidation, sasa tatizo lililopo ni kwamba wafanyabiashara wanapoenda kununua bidhaa kwa mfano China Guangzhou, Uturuki, Dubai, Marekani uwatumia hawa wasafirishaji ambao kwa lugha ya kitaalumu wanaitwa Consolidators’- Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa, Mhe. Juliana Didas Masaburi
‘Na hawa Consolidators kazi yao kubwa ni kukusanya mizigo ya wafanyabiashara na kuweka kwenye kontena moja sasa nachangia hili kwasababu gani kwaajili ya yale yaliyowahi kutokea mwezi uliopita pale Kariakoo’ – Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa, Mhe. Juliana Didas Masaburi
‘Mheshimiwa Mwenyekiti hawa Consolidators ambao wanafanya biashara ya kukusanya mizigo ya wafanyabiashara wadogo wadogo na kuingiza nchini, mfumo huu Serikali ilikuwa na nia njema kabisa ili kukusanya mizigo ya wafanyabiashara lakini Mheshimiwa Waziri wa Fedha Mfumo huu ndio unawasababishia kukosa kodi halisi’- Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa, Mhe. Juliana Didas Masaburi
‘Sababu zilizopo ni kwamba Mfanyabiashara anapoenda China ama Dubai ama popote pale kununua bidhaa anapewa risiti kwenye kisha akienda kwenye magala anakutana na Consolidation kisha mzigo unapofika hapa nyumbani hawa watu wanakwepa suala la kulipa kodi kwani wanatumia majina yao ama kampuni zao kuingia hiyo wanalipia wao wenyewe hiyo mizigo na wakishamaliza kisha wanawapatia wafanyabiashara bila kuwapa risiti zao’- Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa, Mhe. Juliana Didas Masaburi
‘Tatizo linakuja sasa, Afisa TRA anapoenda Kariakoo kukagua mahesabu ya wafanyabiashara ama mizigo tatizo wale wafanyabiashara wanakuwa hawana risiti halisi na ndio maana mnapowaambia masuala ya kodi wanasema wanaonewa kwasababu kiukweli wanakuwa hawana kumbukumbu ya risiti nia ilikuwa njema lakini naona inaenda tofauti na matarajio’- Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa, Mhe. Juliana Didas Masaburi