Mbunge wa Jimbo la Geita Joseph Kasheki Musukuma ameomba Muongozo wa Spika kupitia kanuni ya 76 ya kanuni za kudumu za bunge inayoomba Bunge kusitisha shughuli zake na kujadili jambo la dharura na ameomba kujua hatima ya kinachoendelea katika soko la Kariakoo ambapo hivi karibuni ilisambaa taarifa ya mgomo wa wafanyabiasha katika Soko la Kariakoo na katika baadhi ya majiji nchini ikiekeza kutofungua maduka ifikapo Juni 24,2024(Leo Jumatatu).
“Kumekuwa na kipeperushi kinatembea mitandaoni kuanzia Ijumaa na Jumamosi kuhusiana na wafanyabiashara wa kariakoo na sehemu zingine kufunga maduka Jumatatu ambayo ni leo na tunavyozungumza sasahivi Kariakoo imefungwa hakufanyiki biashara lakini pia sisi wabunge haya mambo tuliyaibua kwenye michango yetu na natambua kamati ya wafanyabiashara iko hapa kwaajili ya kuzungumza na serikali kutatuliwa matatizo yao sasa nilikuwa naomba kauli ya serikali kulingana na kilichopo Kariakoo kwasababu wafanyabiashara wetu wa kijijini wameenda Dar Es Salaam kufuata mahataji wamekuta Kariakoo imefungwa wengine hawana nauli wanaanza kuomba kwetu” Mbunge Musukuma.