Ikiwa imepita siku tatu tangu Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya kaskazini na mbunge wa zamani wa Arusha Godbless Lema kutoa tamko kua kazi ya kuendesha Pikipiki maarufu kama Boda boda ni kazi ya laana ambayo haitikiwi watu kuitukiza na badala yake itafutwe njia nyingine ya vijana hao waajiliwe pengine kwani inaleta vifo,vilema na adha zingine.
Leo katika Mkutano wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Singida ulioitwa na Katibu mkuu wa CCM Daniel Chongolo kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi na kutatua.
Mbunge wa jimbo la Singida Magharibi Elibariki Kingu na Mwenyekiti wa UVCCM Mohammed Kawaida wamemjibu mwanasiasa huyo na kusema kazi ya bodaboda imeajiri vijana wengi zaidi ambayo inawasaidia kumaliza shida zao za kijamii kama huduma kwa familia,kusomesha na mengine mengi hivyo kazi hiyo siyo laana na kuwataka madereva wa bodaboda kuendelea na kazi na kupuuza kauli hizo.