Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe. Salim Alaudin Hasham amewalipia ada ya leseni ya uvunaji wa mazao ya misitu (Mkaa na kuni) Vikundi sita (6) ambavyo vina jumla ya vijana 35.
Akizungumza baada ya kuwakabidhi risiti za malipo ya Vibali hivyo Katibu wa Mbunge Ndg Thomas Daffa Machupa amevitaka vikundi hivyo kufuata sheria za uvunaji wa mazao ya misitu ili waweze kuepuka changamoto za kukamatwa mara kwa mara.
Pia amewataka vijana kutumia fursa hio vyema ili kujiinua kiuchumi kwani nia ya mbunge ni kuona vijana wanaojiajiri wanainuka kiuchumi ikiwa ndio njia mbadala ya kupambana na Changamoto ya ajira.
Nao wawakilishi wa vikundi hivyo wamemshukuru Mbunge Salim Alaudin kwa kutimizia ahadi hio aliyowapatia tangu mwezi wa tano na kusema wataitumia vyema fursa hio kukuza vipato vyao na familia zao ili kuondokana na umaskini.
Jumla ya vikundi sita (6) ambavyo vinavyojishughulisha na biashara hiyo ya mazao ya misitu vimelipiwa kiasi cha shilingi milioni moja na laki sita na ishirini (1,620,000/=) kwani kila kikundi ni 270,000/= tu kwa mwaka mzima.