Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro.Mhe. Salim Alaudin Hasham ameziomba Mamlaka zinazohusika na mikopo ya asilimia 10 ya vijana walemavu na wanawake kuharakisha mikopo ili wananchi wapate mikopo hiyo.
Mhe. Salim ameyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara kijiji cha Minepa baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu mikopo hiyo kutopata licha ya kukamilisha taratibu zote.
Salim amesema kuna haja ya. Serikali kufanya michakato haraka ya mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri ni zaidi ya mwaka mmoja umepita tangu serikali ilivyositisha utolewaji wa mikopo hiyo lakini kumeonekana kuna uhitaji mkubwa sanaa na ilikua mkombozi kwa wananchi kuacha kuwa tegemezi.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya Ulanga Saida Mahugu amesema hadi sasa tayari wametenga milioni mia mbili kwa ajili ya mikopo ya asilimia 10 vijana ,wanawake na walemavu lakini wanasubiri utaratibu kutoka serikali kuu.
Anasema serikali ilisitisha uratibu wa utoaji mikopo hiyo kutokana na wanakikundi wengi kushindwa kurejesha mikopo ambapo kwa halmashauri ya Ulanga pekee kuna zaidi ya milioni mia nane ambazo vikundi vimeshindwa kurejesha na kusababisha wananchi wengine kukosa mikopo.