Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe.Salim Alaudin Hasham amewapatia fedha kiasi cha Shilingi Milioni moja (1,000,000/=) na kuwalimia bure shamba lao lenye jumla ya ekari 20 kwa lengo la kuwainua kiuchumi vijana hao.
Akikabidhi fedha hizo katibu wa Mbunge Ndg Thomas Daffa amesema mbunge amevutiwa na uthubutu wa vijana hao kuamua kurejea shambani ili kujipatia kipato chao cha kila siku na ana imani kuwa vijana hao watainuka kiuchumi na kubadilisha maisha yao.
Abubakari Bolly na Godfrey Malunda ni moja ya vijana waliopata msaada huo wamemshukuru Mbunge kwa jitihada zake za kuwainua wananchi kiuchumi hususani vijana na wameahidi kutekeleza mradi wao wa kilimo kwa nguvu zote ili tija ionekane hapo baadae.
Mbunge Salim anaendelea na zoezi la kuwasaidia wananchi wake hususani wakulima kwani tangu mwezi Septemba mwaka huu ametoa trekta tatu ambazo zinawalimia wananchi bure jukumu lao ni kuweka mafuta tu jambo ambalo limewanufaisha wakulima wa hali ya chini kulima kisasa ili kujipatia mazao kwa wingi.
Hadi sasa Trekta hizo zimeshalima jumla ya ekari 375 na bado zipo mashambani kuendelea na huduma hiyo.